Mengi yamezungumzwa baada ya Bodi ya ligi kutangaza kusogeza mbele mchezo watani wa jadi kati ya Yanga dhidi ya Simba ambao awali ulipangwa kupigwa Oktoba 18
Uamuzi wa kuusogeza mchezo huo Novemba 07 kwa maslahi mapana ya vilabu vyenye wachezaji wa kigeni ambao wanapaswa kusafiri kwenda kuzitumikia timu zao za Taifa wakati huu ambao kuna changamoto ya usafiri wa anga kutokana na janga la corona
Wapo waliodai kuwa mchezo huo umeahirisha eti kwa sababu winga Luis Miquissone ana kadi tatu za njano hivyo hataruhusiwa kucheza
Ukweli ni kwamba Miquissone ana kadi mbili za njao alizopata katika michezo dhidi ya Biashara United na JKT Tanzania
Hivyo hata kama mechi ingebaki Oktoba 18, Miquissone alikuwa na sifa ya kucheza kwani ni kadi tatu za njano zinazoweza kumfanya mchezaji akakosa mchezo mmoja