Simba yaitandika Azam FC 1-0

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Feb 2018
Simba yaitandika Azam FC 1-0
Wekundu wa msimbazi, Simba wameendelea kutimua vumbi kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kuichapa Azam FC bao 1-0 katika mchezo mkali uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa Jumatano jioni.

Emanuel Okwi ameendeleza rekodi yake nzuri ya kufunga mabao kwenye uwanja wa Taifa baada ya kupachika bao pekee la Simba kwenye dakika ya 36 akiunganisha krosi murua ya Asante Kwasi.



Simba iliuanza mchezo huo taratibu, hata hivyo baada ya dakika 15 ilianza kuupiga mwingi kama ilivyofanya kwenye michezo iliyopita.

Matokeo ya ushindi leo yanaiweka Simba kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya alama saba baada ya kufikisha alama 41.



Yanga iko nafasi ya pili ikiwa na alama 34 huku Azam FC ikishushwa hadi nafasi ya tatu ikibaki na alama zake 33 sawa na Singida United iliyo nafasi ya nne.

Ni dhahiri kwa mwenendo wa kikosi cha Simba sasa, haitakuwa kazi rahisi kuizuia isitwae ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

Ushindi dhidi ya Azam ulikuwa moja ya ushindi muhimu kwa kuwa Azam FC ni moja ya timu imara msimu huu zilizo katika mbio za ubingwa.

Aidha Emanuel Okwi nae ameendelea kung'gan'gania kileleni kwenye orodha ya vinara wa mabao baada ya kufikisha mabao 13.

Anafuatiwa na Obrey Chirwa mwenye mabao 10 huku John Bocco na Habibu Kiyombo wakifuata kwenye nafasi ya tatu wakiwa wamefunga mabao 9 kila mmoja.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
47m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’