Baada ya kikosi cha Simba kurejea jijini Dar es salaam hapo jana, kocha Sven Vandenbroeck aliwapa wachezaji mapumziko ya siku chache kabla ya kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya Yanga ambao utapigwa Oktoba 18
Katika mchezo huo wa kwanza utakaowakutanisha watani hao wa jadi msimu huu, Simba watakuwa wageni
Sven aliwapa wachezaji mapumziko ya siku mbili na ataanza mazoezi bila ya wachezaji 11 walioitwa timu za Taifa
Mechi za Kimataifa za kirafiki zitapigwa wiki ijayo Tanzania ikitarajiwa kucheza na Burundi Oktoba 11 katika mchezo ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
ADVERTISE HERE