Rafu za JKT Tanzania zamkera Sven

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Oct 2020
Rafu za JKT Tanzania zamkera Sven

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ameeleza kutofurahishwa na madhambi ya makusudi waliyokuwa wakifanyiwa wachezaji wake kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania ambao ulipigwa mkoani Dodoma jana Jumapili

Katika mchezo huo ambao uliwashuhudia mabingwa wa nchi wakiondoka na ushindi wa mabao 4-0 huku wakicheza kandanda la kuogopesha, kwa nyakati tofauti wachezaji wa JKT Tanzania waliwafanyia rafu mbaya nyota wa Simba waliokuwa wametakata kwelikweli wakilipiga 'pira' la levo za Kimataifa, mhanga mkubwa akiwa Bernard Morrison

Sven amesema wachezaji wake wamekuwa wakikamiwa na timu pinzani hivyo kuna umuhimu kwa waamuzi kuwalinda ili wasije wakaumizwa

"Tulikuwa na mchezo mzuri, nafurahi kuona wachezaji wangu wamefanya kile nilichowaelekeza na muhimu zaidi tumepata matokeo tuliyoyahitaji. Lakini sikufurahishwa na mchezo waliokuwa wakicheza JKT Tanzania dhidi ya wachezaji wangu.

"Nafikiri kuna umuhimu wa waamuzi kuwalinda wachezaji, kwani imekuwa kawaida kwa timu pinzani kukamia wachezaji wetu, wanayo haki ya kulindwa," alisema Sven

Ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania umeirudisha Simba kwenye nafasi ya pili nyuma ya Azam Fc ambayo bado imegoma kudondosha pointi baada ya kupata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Kagera Sugar hapo jana

Β 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
21h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’