Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba, jioni ya leo kitashuka kwenye uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma kuumana na JKT Tanzania katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Simba ilitua Dodoma mapema jana na jioni ikafanya mazoezi yake ya mwisho katika dimba la Jamhuri
Huu ni mchezo muhimu kwa Simba kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu kujiweka kwenye mazingira mazuri kabla ya mchezo dhidi ya watani zao Yanga ambao utapigwa Oktoba 18
Lakini inafahamika, mchezo hautakuwa mwepesi kutokana na mazingira ya uwanja wa Jamhuri
JKT Tanzania ni moja ya timu ngumu zinaopokuwa nyumbani na hata msimu uliopita, JKT Tanzania walipata ushindi dhidi ya Simba katika mchezo wa duru ya pili
Kocha Sven Vandenbroeck amesema wachezaji wake wako tayari kwa mchezo huo ambao anatarajiwa kuucheza kimbinu zaidi
Sven leo anaweza kutumia washambuliaji wawili kwani mazingira ya uwanja hayaruhusu kucheza soka lake la chinichini na pengine atalazimika kutumia mipira mirefu
Mchezo utapigwa kuanzia saa kumi Alasiri