Baadae leo kikosi cha mabingwa wa soka nchini Simba kitashiriki hafla maalum itakayowajumuisha Wanachama na Mashabiki wa klabu ya Simba mkoani Dodoma
Hafla hiyo itatumika kwa Wanasimba wa Dodoma kujipatika kadi za mashabiki kupitia kampeni iliyoanza mkoani Dodoma tangu mwanzoni mwa wiki hii
Simba iliwasili mkoani Dodoma majira ya mchana wakitokea Morogoro ambako walilala likiwa ni ombi la mashabiki wa mkoa huo waliohitaji wapelekewe ubingwa wa Ligi Kuu



ADVERTISE HERE