Maproo waipa mtihani Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Oct 2020
Maproo waipa mtihani Simba

Wachezaji watano wa klabu ya Simba wameitwa kujiunga na timu za Taifa kwa ajili ya michezo ya kirafiki ambayo iko katika kalenda ya FIFA

Nyota hao wanaopaswa kujiunga na timu za Taifa kuanzia Oktoba 05 ni Luis Miquissone (Msumbiji), Francis Kahata (Kenya), Clatous Chama (Zambia), Larry Bwalya (Zambia) na Joash Onyango (Kenya)

Michezo ya kirafiki ya Kimataifa itapigwa kati ya Oktoba 10 na Oktoba 14 kwa wastani wa wiki moja kabla ya mchezo wa watani wa jadi utakaopigwa Oktoba 18

Changamoto iliyopo ni kuwa nyota hao huenda wakashindwa kurejea kwa wakati kuuwahi mchezo dhidi ya Yanga

Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema ni vyema Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) likahakikisha wanapanga ratiba zao kwa kuzingatia kalenda za michezo ya Kimataifa

"Wachezaji wanapaswa kusafiri Oktoba 05 lakini sisi Oktoba 04 tunapaswa kuwa mkoani Dodoma kucheza na JKT Tanzania. TFF wanapaswa kuliangalia hili kwa umakini zaidi huko mbeleni kwani kalenda ya FIFA inafahamika. Ratiba inapaswa kuzingatia kalenda za Kimataifa ili kuwapa nafasi wachezaji kutumikia timu zao za Taifa kwa Uhuru," aisema

Bado kuna changamoto ya usafiri iliyosababishwa na ugonjwa wa corona, Miquissone na Chama walichelewa kujiunga na wenzao mwanzoni mwa msimu kutokana na changamoto hiyo

Hata hivyo uongozi wa Simba umesema wanaamini nyota hao watarejea kwa wakati kuwahi mchezo dhidi ya Yanga na hata wakikosekana haliwezi kuwa tatizo kwao

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
11h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’