Kikosi cha Simba kinaondoka jijini Dar es salaam leo kuelekea mkoani Dodoma kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya JKT Tanzania ambao utapigwa keshokutwa Jumapili kwenye uwanja wa Jamhuri
Mabingwa hao wa nchi wataweka kambi ya siku moja mkoani Morogoro, kesho Jumamosi wataianza safari ya kuelekea Dodoma
Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema mashabiki wa timu hiyo wa mkoani Morogoro waliomba timu ipite Morogoro ili wapate wasaa wa kufurahia ubingwa waliotwaa msimu uliopita
"Kikosi kitaondoka kwa basi kuelekea Dodoma lakini tuna ombi la mashabiki wa Morogoro ambao waliomba tuwapelekee taji letu la ligi ambalo tulitwaa msimu uliopita.
"Hivyo kwa kukubali ombi letu la mashabiki wa Morogoro tutakuwa na kombe letu, mashabiki watapata muda wa kuliona kombe letu na Jumamosi tutaanza safari kuelekea Dodoma ambapo tutapata muda wakufanya mazoezi ya mwisho kabla ya kuikabili JKT Tanzania," amesema.