Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo watakuwa nyumbani kujaribu kuendeleza kasi yao ya ushindi itakapowakaribisha Azam FC kwenye mchezo mkali wa ligi kuu ya Vodacom.
Mchezo huo unaozikutanisha timu mbili zinazochuana vikali kuelekea ubingwa, matokeo yake yatatoa picha halisi juu ya hatma ya ubingwa.
Simba itaingia kwenye mchezo huo ikiwa kwenye kiwango bora baada ya kushinda michezo mitano mfululizo na kufanikiwa kufikisha alama 38.
Azam FC iko nafasi ya tatu ikiwa na alama 33. Imeondolewa kwenye nafasi ya pili na Yanga iliyopata ushindi dhidi ya Njombe Mji jana.
Ingawa matokeo ya aina yoyote hayataiondoa Simba kileleni, ushindi ndio matokeo sahihi kwa vinara hao wa ligi waliodhamiria kutwaa ubingwa mapema.
Kuelekea mchezo huo, kocha msaidizi wa Simba, Mrundi Masoud Djuma amesema kuwa wanaiheshimu Azam kwa kuwa ni moja ya timu bora na ngumu kwenye ligi, lakini anajivunia kasi ya timu yake na utimilifu wa wachezaji wake.
"Itakuwa moja ya mechi nzuri..., lengo letu ni ushindi na tunaujua ubora wa wapinzani wetu upo wapi, lakini nakiamini zaidi kikosi changu," alisema Djuma.
Alisema mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi ambaye alipigwa kiwiko na kulazimika kutoka nje kwenye mchezo uliopita dhidi ya Ruvu Shooting yupo katika ari nzuri.
"Ushindi utatuweka kwenye morali ya juu zaidi kuelekea kwenye mchezo wetu wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho wiki hii," alisema Djuma.
Kwa upande wake, kocha msaidizi wa Azam, Iddi Cheche, alisema kuwa watapambana kujaribu kupunguza pengo la pointi dhidi ya vinara hao.
"Bado tunautaka ubingwa, Simba wametuzidi kwa pointi tano, tunaamini kama tukifanikiwa kushinda na zikabaki pointi mbili tutakuwa tumekoleza kasi yetu ya ubingwa," alisema Cheche.
"Huu ni mpira na katika mpira lolote linaweza kutokea, hivyo hatuiogopi Simba wala timu yoyote kwenye ligi," aliongezea kusema Cheche

ADVERTISE HERE