Serikali yawaonya wanaofanya vurugu viwanjani

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Oct 2020
Serikali yawaonya wanaofanya vurugu viwanjani

Serikali imeliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuchukua hatua kali kwa watakaoendeleza vurugu uwanjani.

Kauli hiyo inakuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu kutokee vurugu za mashabiki wa Yanga waliowafanyia wale wa Simba katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar, kitendo kinachoonekana kujirudia baada ya kuwahi kutokea kabla Dar es Salaam.

Akizungumza na Azam Media jana, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini, Dk Yusuf Singo alisema anajua kuwa tayari taasisi na klabu zilitoa maonyo ila wao kama serikali wameona pia wakemee ili vitendo hivyo vya kuvunja amani visijirudie.

"Tunajua taasisi zinazohusika pamoja na klabu zimekuwa zikitoa maonyo, tunajua pia TFF na BMT walikemea na serikali tunakemea mashabiki wote wanaovunja amani,"alisema.

Alisema kama vitendo hivyo vitajirudia TFF na BMT watumie kanuni na sheria zilizopo kuwachukulia hatua kali kwa wale watakaohusika ili kuvunja utamaduni huo unaotaka kujengeka.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
3h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
3h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
6h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
12h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’