Thamani ya Miquissone usipime!

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
30 Sep 2020
Thamani ya Miquissone usipime!

Kiungo wa kimataifa wa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba ya jijini Dar es Salaa, Luis Miquissone, ametajwa kuwa ndiye mchezaji ghali kwa sasa sokoni kwa Ukanda wa Afrika Mashariki, imefahamika

Ingawa Simba yenye makao makuu yake Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini, haikuwa tayari kutaja kiasi cha fedha ambacho wametumia kumsajili mchezaji huyo wa timu ya Taifa ya Msumbiji, imesema kumuuza kwa Euro 400,000 ambazo ni zaidi ya Sh. bilioni moja bado ni hasara kwao, huku ikieleza inaweza kukubali kukaa mezani kusikiliza ofa kama klabu itakayomhitaji itafika Euro milioni moja (Sh. bilioni 2.6).

Simba ilimsajili nyota huyo wa zamani wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Miquissone akitokea UD Songo ya Msumbiji, ambapo alifunga bao lililowaondoa kwenye mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita, akiwa na klabu hiyo.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema klabu yake ilimsajili Miquissone kwa dau la juu na uamuzi huo ulifikiwa baada ya kuridhishwa na kiwango alichokionyesha kwenye mechi mbalimbali.

Manara alisema waliangalia uwezo wa Miquissone katika mechi mbalimbali alizocheza akiwa na kikosi cha Msumbiji, Mamelodi na UD Songo na kuvutiwa na kipaji chake.

"Tunajivunia kuwa na kikosi imara, kwa sasa Miquissone ndiye mchezaji ghali, na si kwa Simba tu, ni kwa Afrika Mashariki nzima, tumemnunua kwa dau nono, halijawahi kutokea, analipa kwa kile kiwango anachokionyesha," alisema Manara.

Aliongeza klabu mojawapo ya Uholanzi ilionyesha nia ya kumnunua kwa dau la Euro 400,000, lakini Simba haikuwa tayari kumwachia kwa kiasi hicho cha fedha kilichotajwa.

"Kuna mawakala wa klabu moja ya Uholanzi walikuja kufanya mazungumzo na sisi (Simba), tena kwa hela nzuri ya Euro 400,000 ili kumnunua, lakini 'Mo', (Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohamed Dewji) akasema labda walipe Euro milioni moja (Sh. bilioni 2.6), kiasi walichotaka kwetu ingekuwa hasara," Manara alisema.

Aliongeza kiungo huyo ni mali ya Simba na hajasajiliwa kwa mkopo kama baadhi ya klabu nyingine za hapa nchini zinavyoamini.

"Ni mchezaji wetu halali kwa asilimia 100, tena ana mkataba mrefu, hajaja kwa mkopo, thamani yake ni sawa na kikosi kizima cha ...(hakutaka kutaja cha timu gani), tunamshukuru Senzo (Mazingiza- aliyekuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba), alisaidia sana kufanikisha ujio wake, hakuna ambaye anaweza kumpata," Manara aliongeza.

Kiungo huyo alitoa pasi za mwisho tatu kwenye mchezo dhidi ya Biashara United ambapo Simba ilishinda mabao 4-0 na pia alitoa pasi kama hiyo kwa mpira wa kona, Meddie Kagere akifunga kwa kichwa. Hadi sasa ndiye mchezaji anayeongoza kwa pasi za mwisho akiwa nazo nne hadi sasa wakati huu Ligi Kuu ikiwa raundi ya nne.

Mchezaji mwingine ghali anayetajwa katika kikosi cha Simba ni kiungo kutoka Zambia, Clatous Chama, ambaye imeelezwa klabu inayomtaka ijiandae kutoa kiasi cha Sh. bilioni mbili.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’