Zikiwa zimebaki siku 18 kabla pambano wa jadi Simba na Yanga kuchezwa Serikali imeweka wazi kuwa tiketi zitaanza kuuzwa mapema ili kuondoa usumbufu kutokana na idadi kubwa ya mashabiki kutaka kuhudhuria.
Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Singo amesema Serikali inasubiri Bodi ya ligi kupanga viingilio ili waanze kuuza tiketi.
Singo ameongeza kuwa mashabiki wakinunua tiketi mapema itasaidia kupunguza msongomano ambao wakati mwingine unapelekea kusababisha vurugu.
"Tunajua mechi ya watani wa jadi inakaribia hivyo tunataka tiketi zianze kuuzwa mapema na siku moja kabla ya mchezo hazitauzwa tena," amesema Singo.
ADVERTISE HERE