Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' amewataka mashabiki wa Simba kutolipiza kisasi kwa matukio wanayofanyiwa na watani zao Yanga
Mo amesema Wanasimba waonyeshe ukomavu na upendo na kuwa mpira uwe chachu ya kuwaunganisha watu na kuwafanya wawe wamoja
"Wanasimba endeleeni kupendana: nawaomba kwa heshima na taadhima tuonyeshe ukomavu wa upendo, mpira iwe chachu ya kutuunganisha na kutuleta pamoj"
"Tunawaomba mashabiki wetu wasichukue hatua zozote za kulipiza kisasi wala wasifanye fujo ya aina yoyote dhidi ya mtu yoyote. Sisi kama klabu, kama ilivyo kwa Watanzania wote, tunao wajibu wa ulinzi, amani na utulivu wa nchi yetu na umoja, upendo, na mshikamano miongoni mwa wananchi wa Tanzani"
"Tusingependa kabisa ushabiki wa soka uwe chanzo cha chuki, mifarakano na uvunjifu wa amani katika jamii," ameandika Mo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii