Sven amtaka Bwalya akaonyeshe makali mikoani

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Sep 2020
Sven amtaka Bwalya akaonyeshe makali mikoani

Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck, amemuongezea majukumu kiungo wake Mzambia Rarry Bwalya kuhakikisha anaonyesha kiwango kwenye mechi zao za ugenini baada ya kung’ara kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.

Kocha huyo amempa majukumu Bwalya na wachezaji wengine wa kikosi hicho kuhakikisha wanaonyesha uwezo mkubwa katika mechi zao za mkoani kwa ajili ya kuipa timu hiyo matokeo.

Bwalya amekuwa mmoja wa viungo walioonyesha ufundi katika mechi mbili walizocheza dhidi ya Gwambina ambayo alianza na Biashara United Uwanja wa Mkapa, Dar.

Simba watacheza mechi ijayo ya Ligi Kuu Bara Oktoba 4, dhidi ya JKT Tanzania katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Sven amesema kuwa anataka kuwaona wachezaji wake wote wakicheza kwa kiwango kikubwa kutokana na wengi kuwa na uwezo mkubwa.

"Wiki ijayo tunatoka kwenda ugenini dhidi ya JKT Tanzania, natarajia tutacheza hivihivi kwa kiwango kizuri hata kama kiufundi hatutacheza kama mechi iliyopita dhidi ya Gwambina.

"Lakini natarajia tunatakiwa kupambana kwa nguvu kama mechi zetu mbili zilizopita na uzuri ni kuwa tuna watu wengi wa kufunga mabao," alisema

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
21h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’