Tumeimarika kufunga kupitia mipira ya adhabu - Sven

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Sep 2020
Tumeimarika kufunga kupitia mipira ya adhabu - Sven

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema anafurahishwa na kuimarika kwa wachezaji wake katika matumizi ya mipira ya adhabu kufunga mabao

Juzi beki kiski Paschal Wawa alifunga bao maridhawa kupitia mpira wa adhabu

Lakini pia kona ya Luis Miquissone ilizaa bao la kwanza la Simba likiwekwa kambani na Meddie Kagere katika mchezo ambao Simba iliondoka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Gwambina Fc

Sven amesema ni jambo jema wanaanza kunufaika na mipira ya adhabu kwani katika mechi za nyuma wametumia mipira hiyo mara chache sana

"Wachezaji wanazidi kuimarika kila leo ni jambo zuri na linafurahisha hasa ukizingatia kwamba wameanza kufunga kwa kutumia mipira ya adhabu.

"Wawa amefunga bao moja mbele ya Gwambina kwa faulo, ni mpigaji mzuri na kwetu sisi ni furaha kwani awali ilikuwa ngumu kufunga kwa adhabu, mechi zetu zilizopita tulishindwa na ninaamini hii ni mara ya kwanza.

"Hata Luis Miqussone naye alipiga kona ambayo ilifungwa na Meddie Kagere hivyo kuna maendeleo ambayo yameanza kuonekana ndani ya kikosi kwa sasa tofauti na awali," alisema Sven

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’