Baada ya ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Gwambina Fc, mabingwa wa nchi Simba wanaianza awamu ya pili ya mechi za mikoani
Oktoba 04 Simba itakuwa kule mkoani Dodoma kuumana na JKT Tanzania ingawa mchezo huo unaweza usipigwe Dodoma kama JKT watashindwa kutimiza masharti yaliyotolewa na Bodi ya Ligi ili uwanja huo uendelee kuchezewa mechi za ligi
Wakitoka Dodoma, Simba watasafiri moja kwa moja mkoani Rukwa kuikabili Tanzania Prisons katika mchezo ambao unaweza kupigwa Oktoba 10 uwanja wa Nelson Mandela
Hata hivyo timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Oktoba 11 inaweza kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Burundi, hivyo upo uwezekano mkubwa mchezo huo ukaahirishwa
Mchezo utakaofuata utakuwa jijini Dar es salaam, dhidi ya Yanga Oktoba 18. Hii itakuwa mechi ya kwanza ya dabi msimu huu