Manara alaani tukio la Mashabiki wa Yanga Morogoro

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Sep 2020
Manara alaani tukio la Mashabiki wa Yanga Morogoro

Jana baadhi ya mashabiki wa Simba walifanyiwa vurugu na mashabiki wa Yanga mkoani Morogoro katika mchezo wa ligi kuu kati ya Mtibwa Sugar dhidi ya Yanga

Umekuwa utamaduni kwa vilabu vya Simba na Yanga kuwa siku zote mashabiki wa moja ya timu, mpinzani wake anapocheza huingia uwanjani kushangilia timu pinzani

Lakini inashangaza sana kwa siku za karibuni mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiwafanyia vurugu mashabiki wa Simba wanaoingia katika mechi zao licha ya wao kutofanyiwa hivyo wanapoingia kwenye mechi za Simba

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amelitaka shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na Jeshi la Polisi kuchukua hatua kukomesha matukio hayo yanayohatarisha Amani

"Mategemeo yetu ni kuona TFF inachukua hatua stahiki kwa hivi vitendo vinavyoendelea kufanywa na baadhi ya Washabiki wa Yanga na pia tunatarajia kuona Jeshi letu imara la Polisi mkoa wa Morogoro linaaema kitu kuhusu kadhia ya jana iliyoacha doa kubwa katika amani na usalama kwenye viwanja vya soka nchini"

"Lakini nawasihi Wanasimba msilipe kisasi na muendelee kuhubiri na kutenda yaliyo mema viwanjani, endeleeni kufurahia burudani viwanjani, mengine tuwaachie TFF na Polisi kwa hatua zao kwa mujibu wa sheria zilizopo. Simba ni klabu ya watu wastaarabu na kamwe tusishiriki hata kwa bahati mbaya mambo ya hovyo hovyo," amesema Manara

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’