Kahata ajipanga upya Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Sep 2020
Kahata ajipanga upya Simba

Kiungo mshambuliaji wa Simba Francis Kahata amesema ushindani wa namba ndani ya kikosi cha Simba umeongezeka kutokana na kila nafasi kuwa na wachezaji wenye viwango vya juu

Tangu kuanza kwa msimu huu Kahata hajafanikiwa kupata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kocha Sven Vandenbroeck na wakati mwingine ameshindwa kuingia katika kikosi cha wachezaji 18

Pamoja na changamoto hiyo Kahata amesema anayafurahia maisha ndani ya kikosi cha Simba na ataendelea kupambana ili kupata nafasi ya kuanza.

"Kila mchezaji anayecheza anacheza kwa ajili ya timu, na timu ikishinda tumeshinda wote, ushindani ni mkubwa lakini hali hiyo ni nzuri kwa wachezaji kwa sababu inakuwa ni changamoto kwa kila mchezaji kuongeza juhudi mazoezini.

"Mwanzoni mwa msimu sikuwa fiti kwani nilipata majeraha ingawa sasa yamepona na nipo fiti kucheza, lakini ushindani wa namba ni mkubwa na hilo ndilo linalotakiwa, sina wasiwasi najua nitacheza tu," alisema Kahata

Ujio wa wachezaji Bernard Morrison na Larry Bwalya umepelekea Mkenya huyo kutokuwa na uhakika wa kuanza kama ilivyo kwa Miraji Athumani na Hassan Dilunga

Nyota huyo wa Kimataifa wa Kenya amesema anaamini ni muda tu unahitajika na kuongeza juhudi mazoezini ili kumshawishi Kocha Mkuu Sven Vandenbroeck kumpanga katika kikosi cha kwanza

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
4h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
10h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
13h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’