Simba imeendelea kuwanyanyasa wapinzani wake uwanja wa Benjamini Mkapa baada ya kuichabanga Gwambina Fc mabao 3-0
Gwambina waliingia na mbinu ya kupaki basi hata hivyo walishindwa kuhimili presha ya Simba iliyojipatia bao la kuongoza kwenye dakika ya 42 kupitia kwa Meddie Kagere 'MK14'
Kagere anafunga bao la pili katika mchezo wa pili mfululizo
Simba ikaongeza bao la pili dakika tano baada ya kuanza kipindi cha pili, kupitia mpira wa adhabu uliowekwa kambani na Sultan Paschal Wawa
Katika mchezo huo ni Simba iliyokuwa kila mahali, umahiri wa mlinda lango wa Gwambina, uliwanusuru vijana hao wa kanda ya ziwa kuondoka na kapu la mabao
Umeanza kuwa utamaduni kwa mshambuliaji Chris Mugalu kufunga katika kila mchezo, leo akiingia kambani kwa mara ya nne katika mchezo wa nne aliocheza
Mugalu amefunga mabao manne katika mechi nne alizocheza, mabao matatu akiyafunga akitokea benchi

Huu ni mtambo mwingine wa mabao umetua Msimbazi
Ushindi huo umeipandisha Simba mpaka nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 10