Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba usiku wa leo majira ya saa moja watashuka kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Gwambina Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Huu ni mchezo wa mzunguuko wa nne, ukiwa wa pili kwa Simba kucheza kwenye uwanja wake wa nyumbani
Wiki iliyopita mabingwa hao wa nchi waliifumua Biashara United mabao 4-0
Wanapocheza katika uwanja wao wa nyumbani, Simba 'wananoga' kwelikweli, Gwambina wanapaswa kujipanga hasahasa kwani haitakuwa kazi rahisi kuwadhibiti wababe hao wa soka hapa nchini
Kimahesabu Simba inaweza kupanda kileleni mwa msimamo wa ligi kama itapata ushindi dhidi ya Gwambina leo na Azam Fc ikishindwa kuondoka na alama tatu dhidi ya Tanzania Prisons kule Rukwa
Ni baada ya vinara wa ligi hiyo KMC jana kuangukia pua kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Kagera Sugar
Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo huo huku akiahidi burudani kwa mashabiki
Ni saa mija jioni pale uwanja wa Benjamin Mkapa