Keshokutwa Jumamosi, Septemba 26, saa moja usiku kero zinaendelea pale uwanja wa Benjamin Mkapa wakati mabingwa wa nchi Simba watakaposhuka uwanjani kumenyana na Gwambina Fc
Ni mchezo wa ligi kuu ya Vodacom raundi ya nne
Bei ya viingilio vya mchezo huo, VIP A ni Tsh 15,000/-, VIP B ni Tsh 10,000/-, VIP C ni Tsh 5,000/- na Mzunguuko ni Tsh 3,000/-
Simba imeainisha maeneo ambayo tiketi zinapatikana huku wakiwataka mashabiki kuhakikisha wanakata tiketi zao mapema kuepuka usumbufu wowote unaoweza kujitokeza siku ya mchezo

ADVERTISE HERE