Mugalu afurahia kufunga mechi ya kwanza VPL

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Sep 2020
Mugalu afurahia kufunga mechi ya kwanza VPL

Mshambuliaji wa Simba Chris Mugalu aliyesajiliwa na mabingwa hao wa nchi akitokea Lusaka Dynamos ya Zambia, amesema kuwa amefarijika baada ya kufunga katika mchezo wake wa ligi kuu 

Mugalu aliifungia Simba bao la nne katika ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Biashara, mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar.

Mcongomani huyo amesema kuwa anafurahi kuona amefunga bao katika mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu ambapo anaamini kufanya hivyo kutampa hali ya kujiamini kwa kufanya vizuri katika michezo inayofuata

Aidha amempongeza kiungo fundi Clatous Chama kwa kumtengenezea nafasi maridhawa kwa pasi ya kisigino

"Nimefurahi kufunga katika mchezo wangu wa kwanza wa ligi hii itaniongezea kujiamini katika michezo yangu inayofuata kucheza kwa kujiamini, ukiwa kama mshambuliaji lazima udaiwe mabao hivyo kama hautafunga basi utacheza kwa wasiwasi lakini kwangu nashukuru nimefunga,"alisema

"Kuhusu pasi ya Chama nimefurahi kuona kanipa pasi nzuri, nilikuwa nimekaa sehemu nzuri ya kufunga lakini sikutarajia kama Chama angenipigia pasi kama ile,ila nashukuru kwa kuwa alinipa na nikafunga"

Mugalu amefunga mabao matatu tangu alipojiunga na Simba, moja kwenye ligi na mawili kwenye mechi za kirafiki dhidi ya Vila'o na African Lyon

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
13h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
17h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
23h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’