Wakati mkataba wake ukitarajiwa kumalizika mwezi Julai 2021, kocha mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ameutaka uongozi wa Simba umuongeze mkataba Mzambia Clatous Chama
Chama ameanza msimu akiwa na kiwango cha juu juzi akiingoza Simba kuibomoa Biashara United mabao 4-0, akifunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya bao
Mbelgiji huyo amesema anadhani ni sahihi Chama kuongezewa mkataba wakati huu kwani kwa ubora alionao, timu nyingi zinaweza kuongeza ushindani wa kumuwania pale mkataba wake utakapomalizika
"Binafsi ningefurahi kumbakisha kwa kiwango anachoendelea kukionesha kwa sasa, kama kocha ninafuraha kuwa naye sehemu ya kikosi, ana ubunifu na anafanya kazi inayotakiwa, sio kwa mimi ni kwa kocha yeyote hawezi kuona mchezaji mzuri anaachwa," amesema Sven
"Kikubwa mimi kama kocha sina maamuzi makubwa, ila yapo mikononi mwa timu na mchezaji mwenyewe, siwezi kujua anachowaza Chama au Bodi ya Simba, wanachofikiria kwa sasa juu ya kumuongeza mkataba"
Inaelezwa tayari uongozi wa Simba umeanza mazungumzo na Wakala wake ili wamuongezee mkataba juu ya ule utakaomalizika mwezi Julai 2021
Hata hivyo Mzambia huyo amewataka mabosi wake wasubiri wakati mwafaka atamwaga wino