Jana Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez akiongozana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, Mulamu Nghambi walitembelea makao makuu ya klabu ya Al Ahly yaliyopo jijini Cairo, Misri
Kulingana na taarifa iliyotolewa na klabu ya Simba mapema leo, Al Ahly na Simba zimekubaliana kushirikiana kwenye maeneo ya biashara, ufundi na uendelezaji wa wachezaji kwa kujenga kituo cha kukuza vipaji


Kituo hicho kitakuwa cha kwanza kujengwa nje ya Misri (barani ya Afrika) ambacho kitaendeshwa na Simba na Al Ahly
Aidha, miamba hao wa soka Barani Afrika hapo baadae watakuja nchini kucheza mchezo wa kirafiki na Simba
ADVERTISE HERE