Mashabiki wengi wa Simba walijitokeza kushuhudia mchezo dhidi ya Biashara United jana lakini wakakosa nafasi ya kuingia kutokana na changamoto ya mfumo mpya wa kadi
Uongozi wa klabu ya Simba unapaswa kufanyia kazi changamoto hii ambayo kwa hakika siku ya jana imewakosesha mapato mengi mno
Tangu kuanza kwa matumizi ya mfumo huo, changamoto zimekuwa nyingi, mashabiki wanafika uwanjani lakini wanashindwa kuingia uwanjani
Aidha kwa mashabiki nao ni vyema tukaacha ule utamaduni wa kwenda kukata tiketi uwanjani
Matumizi ya teknolojia yamerahisisha sana, unaweza kukata tiketi yako mapema ili kuepuka usumbufu uwanjani
ADVERTISE HERE