Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ameeleza kuridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wake jana kwenye mchezo dhidi ya Biashara United ambao Simba walifanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 4-0
Sven amesema vijana wake walionyesha dhamira ya ushindi tangu dakika ya kwanza, Biashara United wana bahati kwani walistahili kufungwa zaidi ya mabao manne
"Sina mengi ya kuzungumza zaidi nawapongeza wachezaji wangu kwa mchezo mzuri. Tuliuchukua mchezo tangu dakika ya kwanza, tulikuwa bora zaidi kimbinu kuliko wapinzani wetu. Pengine tulistahili kufunga mabao zaidi"
"Huu ulikuwa mchezo muhimu sana kwetu kushinda katika uwanja wetu wa nyumbani, zaidi nimefurahi hatukuruhusu bao," alisema Sven
Mbelgiji huyo amesema watahakikisha wanaendeleza wimbi la ushindi katika michezo mingine, mchezo unaofuata ukiwa dhidi ya Gwambina Fc Jumamosi ijayo
Katika mchezo wa jana, Simba ilipiga mashuti langoni langoni kwa Biashara United, mabao manne yakafungwa lakini kulikuwa na nafasi za wazi ambao pengine zingeipa Simba mabao mengine manne