Mabingwa wanarejea nyumbani leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
20 Sep 2020
Mabingwa wanarejea nyumbani leo

Wekundu wa Msimbazi, Simba leo wako uwanja wa nyumbani Benjamin Mkapa wakiwakaribisha Biashara United katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom ambao utapigwa kuanzia saa moja usiku

Huu ni mchezo wa kwanza kwa mabingwa hao watetezi kucheza katika uwanja wao wa nyumbani wakianzia mkoani Mbeya na baadae kuelekea Morogoro

Shoo ya kibabe imeandaliwa kwa ajili ya mashabiki hivyo wameaswa kujitokeza kwa wingi pale kwa Mkapa

Viingilio vya mchezo huo ni rafiki kabisa ambapo VIP ni Tsh 15,000/-, VIP B ni Tsh 10,000/-, VIP C ni Tsh 5,000/- na Mzunguuko ni Tsh 3,000/-

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema leo wana kila sababu ya kupata ushindi katika mchezo huo unaopigwa kwenye uwanja waliouzoea

"Mashabiki watarajie burudani nzuri kwani tutakuwa nyumbani tena katika uwanja wetu utakaotupa Uhuru wa kucheza vile tulivyozoea," alisema

Sven amejiwekea malengo ya kuhakikisha timu yake inashinda mechi tano na kuwa kileleni kabla ya mchezo dhidi ya Yanga Oktoba 18

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
12h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’