Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo kimekamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Biashara United ambao utapigwa kesho Jumapili, uwanja wa Benjamin Mkapa, saa moja jioni
Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi, kuiunga mkono timu yao katika mchezo huo wa kwanza nyumbani msimu huu
"Tutacheza nyumbani na hiyo ni faida kwetu. Tunaenda kwenye uwanja wa Mkapa ambao unatupa nafasi ya kucheza vizuri, tumejiandaa kufanya vizuri," amesema







ADVERTISE HERE