Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ameeleza kuyasikia maoni ya mashabiki kuhusu kikosi chake hata hivyo amesema ataendelea kusimamia kile anachokiamini
Sven amesema sio jambo baya kwa mashabiki kutoa maoni yao lakini yeye kama kocha ni lazima aangalie ni namna gani timu yake inapaswa kucheza ili kupata matokeo
"Maoni ya mashabiki sio mabaya, mfumo wowote tunaweza kutumia, inaweza kuwa 4-4-2 au 4-3-3 lakini mwisho wa siku benchi la ufundi tunapaswa kufanya kile tunachokiamini na chenye manufaa kwa klabu," alisema Sven
Mbelgiji huyo amewataka mashabiki na wadau wa soka kuwa watulivu, hawapaswi kumpangia timu kwani anafahamu ni mchezaji gani amtumie wakati gani
Kumekuwa na mjadala mkali miongoni mwa wadau kuhusu kutopangwa kwa mshambuliaji Meddie Kagera ambapo mapema wiki hii Meneja wake Patrick Gakumba alimtahadharisha Sven kuwa uamuzi wake wa kutomtumia Mnyarwanda huyo unaweza kumgharimu
Baada ya mechi mbili za mikoani, kikosi cha Simba kitashuka uwanja wa Banjamin Mkapa kesho Jumapili kuumana na Biashara United