Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema kuwa wanaweza kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kama watashinda michezo yote mitano ijayo
Mchezo wa kwanza utapigwa keshokutwa Jumapili kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Biashara United
Baada ya wiki moja Simba iterejea tena uwanja wa Mkapa kuikabili Gwambina Fc
Mechi nyingini ni dhidi ya JKT Tanzania, Prisons na Yanga
"Ninataka kuona timu yangu inapata ushindi wa michezo mitano ijayo ya ligi, ninaamini haitakuwa rahisi lakini nitapambana kufanikisha hilo," alisema Sven
"Wachezaji wanafahamu melengo tuliyojiwekea, najua tutakutana na upinzani mkubwa lakini tunahitaji kuwa juu ya msimamo wa ligi kabla ya kukutana na Yanga"
Mchezo dhidi ya Yanga utapigwa Oktoba 18 katika uwanja wa Benjamin Mkapa