Mapema wiki hii Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilitangaza kuwachukulia hatua Msemaji wa Simba Haji Manara, Mjumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji Zacharia Hans Poppe na Msemaji wa Yanga Hassan Bumbuli kutokana na makosa ya kinidhamu waliyofanya wakati wa shauri la Bernard Morrison
Manara alimalizana na TFF jana kwa kuwasilisha fedha taslim kitita cha Tsh Milioni tano Makao Makuu ya Shirikisho hilo
Manara ni mmoja wa wadau wa klabu ya Simba waliosimama kidete wakati wa sakata hilo kuhakikisha haki inatendeka na mpaka leo Morrison amehalalishwa kuitumikia klabu ya Simba
ADVERTISE HERE