Sven atumie washambuliaji wawili - Nemes

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
17 Sep 2020
Sven atumie washambuliaji wawili - Nemes

Aliyewahi kuwa mlinda lango wa Simba, Steven Nemes, ameonya kuwa timu hiyo ikiendelea kutumia straika mmoja, itapata tabu sana kupata ushindi kwenye mechi zake za Ligi Kuu Tanzania Bara, badala yake inatakiwa itumie mastraika wawili

Mkongwe huyo ametoa maoni yake kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck anafanya makosa kumchezesha straika mmoja mbele jambo ambalo anaifanya timu yake kupata tabu sana ya kushinda, kwa sababu tayari baadhi ya makocha wameshagundua mbinu yake.

"Kwanza kabisa kuchezesha straika mmoja ni lazima awe na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kukaa nao kwa sekunde kadhaa, mwenye nguvu ya kuweza kukabiliana na mabeki wawili au watatu wa timu pinzani, na pia asiwe anatoka sana kwenye eneo la goli kwenda kutafuta mpira sehemu nyingine," Nemes amenukuliwa na gazeti la Nipashe.

Aliongeza kuwa Bocco, pamoja na kuwa na sifa ya kukaa na mpira na nguvu, lakini ana tabia ya kutoka kwenda nyuma, kati na pembeni, hivyo eneo la kati linakuwa halina mtu, hivyo safu hiyo ya ushambuliaji inapwaya.

"Kama Bocco akiwa na Kagere, basi mmoja anatoka kwenda pembeni au kati, lakini mmoja anabaki eneo la hatari na hii huwa inawasaidia sana Simba kupata ushindi tena wa mabao mengi, lakini hii ya straika mmoja inakuwa na matatizo kwa sababu, hata viungo ambao wamewekwa ili wamsaidie kumlisha straika mmoja, nao bado hawafanyi kazi yao vizuri, hilo ni tatizo," alisema.

Nemes pia alisema kwenye mechi za mikoani ambako viwanja si vizuri sana ndiyo tatizo linakuwa kubwa zaidi, hivyo angalau awe hivyo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, lakini viwanja vya mikoani straika mmoja ni tatizo zaidi kutokana na staili ya ucheza wa Simba, hivyo kumtaka kocha huyo abadilike kama anataka kutetea ubingwa wao.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’