Beki kisiki Paschal Wawa amerejea kikosini baada ya kumaliza fungate akitokea kufunga ndoa mwezi uliopita
Wakati akikosekana mkongwe huyo, kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck aliwatumia Joash Onyango na Kennedy Juma kama chaguo lake la kwanza la walinzi wa kati
Hata katika mchezo uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar, Sven aliendelea na walinzi hao licha ya Wawa kurejea

Onyango, Kennedy, Wawa, Nyoni na Ame ndio walinzi wa kati wa kikosi cha Simba msimu huu
Wapo wanaoamini pacha ya Wawa na Onyango itakuwa bora zaidi huku wengine wakiwa wanaamini bado Nyoni na Wawa wanaweza kuendeleza pale walipoishia msimu uliopita

Je ni pacha ipi ya safu ya ulinzi unadhani itakuwa bora na yenye mafanikio zaidi kwa kikosi cha Simba msimu huu?
Wakati ni huu kwa kocha Sven kuweka sawa combination zake kabla ya kuanza kwa michuano ya ligi ya mabingwa mwezi Novemba