Gakumba asikitika Kagere kukosa nafasi Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Sep 2020
Gakumba asikitika Kagere kukosa nafasi Simba

Patrick Gakumba ambaye ni Meneja wa mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere, ameeleza kutofurahishwa na mteja wake kutopata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha Simba

Tangu mwishoni mwa msimu uliopita, Kagere amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi kwenye kikosi cha kocha Sven Vandenbroeck licha ya kuwa Mnyarwanda huyo ndiye mfungaji bora ligi kuu kwa misimu miwili mfululizo

Gakumba amesema Kagere amewapa furaha mashabiki wa Simba kwa misimu miwili aliyowatumikia lakini sasa hajisikii furaha kuona haaminiwi na kocha

Amesema bado Kagere vizuri na anaweza kuwa msaada mkubwa kwa Simba lakini anaheshimu maamuzi ya kocha katika kuamua nani ampange kwenye mechi ipi

"Naheshimu uamuzi wa kocha lakini naamini mteja wangu bado ana nafasi ya kucheza kwenye klabu ya Simba. Kagere amewapa furaha mashabiki wa Simba kwa miaka miwili, sasa wanapokosa furaha wanayohaki ya kuhoji kwa nini mambo yako hivyo," alisema Gakumba

Mara kadhaa Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesisitiza kuwa washambuliaji wake wote ni wazuri lakini kwa sasa atamtumia nahodha John Bocco kama mshambuliaji chaguo la kwanza

Kumekuwa na shinikizo kutoka kwa mashabiki wakimtaka Sven arejeshe mfumo wa zamani wa kutumia washambuliaji wawili kwani mfumo wa mshambuliaji mmoja hauonekani kuwa na faida kubwa kwa Simba hasa kutokana na idadi ndogo ya mabao yanayofungwa sasa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
2h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
20h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’