Kasi ya upachikaji mabao ya John Bocco imeanza kumtisha pacha wake Emanuel Okwi anayeongoza kwa sasa kwenye mbio za kiatu cha dhahabu.
Okwi ana mabao 12 huku Bocco akifikisha mabao 9 baada ya kutupia mabao mawili kwenye mchezo wa jana dhidi ya Ruvu Shooting.
Tangu awe timamu kiafya, Bocco ambaye ndiye nahodha wa kikosi cha Simba amekuwa akifunga kwenye karibu kila mchezo na kuifanya Simba iwe moto wa kuotea mbali.
Aidha ushindani baina ya wawili hao unaonekana kuinufaisha Simba inayosaka ubingwa baada ya kuukosa kwa misimu mitano.
Kuelekea mchezo dhidi ya Azam FC keshokutwa, Bocco amesema ataendeleza rekodi yake ya kupachika mabao bila kujali anakwenda kucheza na timu aliyoitumikia kwa zaidi ya miaka 10.
Bado haijafahamika kama Okwi atakuwa tayari kuivaa Azam FC keshokutwa baada ya kuumizwa hadi kupoteza fahamu jana.
Afisa habari wa Simba, Haji Manara amethibitisha kuwa hali yake inaendelea vizuri na kama madaktari wataridhishwa nae, atajumuishwa kambini kujiandaa na mchezo huo.

ADVERTISE HERE