Nahodha wa Simba John Bocco anaamini timu itarejea katika makali yake karibuni baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar juzi
Mshambuliaji huyo mkongwe amesema waliingia kwenye mchezo huo wakiwa na lengo la kupata ushindi lakini wamekubaliana na kilichotokea
"Nadhani kila mmoja aliona haukuwa mchezo rahisi, tulikuwa na malengo ya kushinda lakini wapinzani wetu nao walijipanga na kuufanya mchezo kuwa mgumu"
"Tulikuwa na nafasi ya kufunga mabao zaidi hatukuweza kuzitumia. Muhimu tunachukulia matokeo kama changamoto na tutasahihisha makosa kwenye mchezo ujao," alisema Bocco
Mchezo unaofuata wa Simba dhidi ya Biashara United na utapigwa Jumapili ijayo kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam
Huu ni mchezo ambao mabingwa hao wa nchi watahitaji kushinda ili kurejesha furaha ya mashabiki wake