Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amekasirishwa na kitendo cha wachezaji Ruvu Shooting kucheza kindava.
Jana Simba ilifanikiwa kuishinda Shooting kwa mabao 3-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara huku mchezaji wake Emmanuel Okwi akitolewa nje baada ya kuumizwa.
Okwi ambaye ni kinara wa mabao Ligi Kuu Bara, aliumizwa na beki Mau Bofu wa Ruvu Shooting kwa kumpiga kiwiko. Bofu alitolewa kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja licha ya kuwa tayari alikuwa na kadi ya njano.
Γ’β¬ΕHuu si mchezo wa kiungwana, hawa watu wanakuwa kama vile wametumwa au wanafanya hivyo kuwaridhisha watu fulani.
Γ’β¬ΕHii si sahihi, inaonekana leo waliingia uwanjani wakiwa wamepania kuwaumiza wachezaji fulani walioambiwa. Si sawa hata kidogo,Γ’β¬Β alisema Hans Poppe ambaye ni mwanajeshi mstaafu.

ADVERTISE HERE