Kiungo wa Simba Mzamiru Yassin ameanza msimu vizuri akizifumania nyavu katika kila mchezo kwenye mechi mbili ambazo Simba imecheza mpaka sasa
Alifunga kwenye mchezo dhidi ya Ihefu Fc na jana akawafunga waajili wake wa zamani Mtibwa Sugar katika mchezo uliomalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Baada ya kufunga bao mkoani Morogoro jana, Mzamiru hakushangilia bao hilo mwenyewe akitaja sababu ni kuwapa heshima waajili wake hao wa zamani
Mzamiru amefichua kuwa wakati yuko katika klabu hiyo, aliishi vizuri na kila mmoja na hata alipoondoka mwaka 2017 kujiunga na Simba, uongozi wa Mtibwa Sugar walimpa baraka zote
Ni kawaida kwa wachezaji wakati mwingine kuamua kutoshangilia pale wanapozifunga timu zao za zamani
ADVERTISE HERE