Mchezo umemalizika uwanja wa Jamhuri kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Mzamiru Yassin alitangulia kuifungia Simba bao la kuongoza kwenye dakika za majeruhi kuelekea mapumziko lakini Mtibwa Sugar wakarejea mchezoni dakika moja tu tangu kuanza kipindi cha pili kupitia bao la Boban Zirintusa
Simba haikuwa na mchezo mzuri sana leo kama ilivyozoeleka mashabiki wakimshushia lawama kocha Sven Vandenbroeck kwa namna alivyopanga kikosi chake
Mfumo wa kutumia mshambuliaji mmoja, umeendelea kulalamikiwa, wengi hawaridhishwi na kutotumiwa kwa mfungaji bora wa misimu miwili mfululizo, Meddie Kagere
ADVERTISE HERE