Vijana wako tayari kuikabili Mtibwa Sugar - Sven

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Sep 2020
Vijana wako tayari kuikabili Mtibwa Sugar - Sven

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wamekamilisha maandalizi yao ya mwisho jioni ya leo kwenye uwanja wa Jamhuri tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa kesho Jumamosi

Akizungumza baada ya mazoezi hayo, Mkufunzi wa Simba Sven Vandenbroeck amesema vijana wake wako tayari kwa mchezo

Aidha Sven amedokeza kuwa kesho anaweza kufanya mabadiliko kadhaa kwenye kikosi chake kutegemeana na mfumo ambao ataamua kuutumia

"Kila mmoja yupo tayari kwa mchezo. Kwangu ni muhimu kuanza vizuri katika michezo ya mwanzoni ili kuwa juu kwenye msimamo kabla ya kwenda kucheza ligi ya mabingwa,

"Mabadiliko yatakuwepo kama sio ya nafasi labda kwenye namna ya uchezaji lakini bado sijaamua," alisema Sven

Naye hahodha wa Simba John Bocco, amesema hawatawadharau Mtibwa Sugar, watacheza mchezo huo kwa nguvu kuhakikisha wanaondoka na alama zote tatu

"Tunawasheshimu wapinzani wetu lakini tutapambana kwa ajili ya timu ili tupate alama tatu"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
8h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
12h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’