Tumefuata alama tatu Morogoro - Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Sep 2020
Tumefuata alama tatu Morogoro - Manara

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amesema mabingwa wa nchi wako mkoani Morogoro kuchukua alama tatu dhidi ya Mtibwa Sugar

Simba ilitua Morogoro mapema jana tayari kwa mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa kesho Jumamosi kwenye uwanja wa Jamhuri

Tambo zimekuwa nyingi kutoka kwa Afisa Habari wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru kuwa Simba wasitarajie kupata matokeo kwenye mchezo huo

Manara amesema Simba ya sasa sio ya kubishana na Mtibwa Sugar, akiwahakikishia mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanja wa Jamhuri siku ya kesho kupata burudani kutoka kwa Machampioni wa Taifa hili

"Sisi hatuna maneno mengi kazi yetu itaonekana uwanjani. Nadhani hakuna mwenye shaka juu ya uimara wa kikosi chetu, hivyo nyie njooni kwa wingi uwanja wa Jamhuri mje mshuhudie burudani kutoka kwa mabingwa," alisema

Baada ya kutua jana mchana, Simba ilianza maandalizi katika uwanja wa Jamhuri

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
46m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’