Kiungo fundi aliyesajiliwa na klabu ya Simba kutoka Lusaka Dynamos ya Zambia, Larry Bwalya amesema ujio wake Simba umelenga kuwa sehemu ya historia ya mabingwa hao wa nchi
Aidha nyota huyo wa Chipolopolo amesema alichofuata yeye ni mataji na atahakikisha mchango wake unafanikisha jambo hilo
Bwalya amesema Simba ni moja ya timu kubwa barani Afrika kwa wakati huu hivyo ni heshima kwake kucheza katika klabu hiyo
"Tangu nitue hapa Simba najisikia niko nyumbani na nitapambana zaidi kuona timu inafanya vizuri. Nina shauku ya kuwa sehemu ya moja ya timu ambayo ilifanya vizuri na kuwa na mafanikio kwa kutwaa mataji kwenye klabu hii ambayo ni moja ya timu kubwa kwa sasa Afrika," alisema
Bwalya tayari ameanza kufurahia mataji ndani ya klabu ya Simba kwani alikuwa sehemu ya kikosi kilichotwaa Ngao ya Jamii kule mkoani Arusha
Yuko mkoani Morogoro na mabingwa hao wa nchi tayari kuivaa Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa ligi kuu siku ya Jumamosi
