Mo yupo saana Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Sep 2020
Mo yupo saana Simba

Wakati Simba ikitarajia kuiwakilisha tena Tanzania Bara katika mashindano ya kimataifa ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu hiyo, Mohammed Dewji 'Mo', amesema hataacha kuwekeza ndani ya timu hiyo licha ya kukutana na changamoto mbalimbali

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mo, alisema kuwa hafikirii kuondoka katika klabu hiyo na ataendelea kuhakikisha inapata mafanikio, huku mabadiliko ya mfumo wa uendeshwaji yakiendelea kufanyiwa kazi.

Mo alisema Simba ni timu anayoipenda kwa dhati na ataendelea kuweka fedha zake kwa sababu ya kusaka mafanikio kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa.

Alisema kwa sasa bajeti ya Simba kwa mwaka ni Sh. bilioni saba na mwaka huu alitumia kiasi cha bilioni 1.9 kwa ajili ya kusajili wachezaji wa timu hiyo.

Alieleza kuwa hafikirii kuondoka katika klabu hiyo ya Wekundu wa Msimbazi labda pale wanachama wa klabu hiyo watakapohitaji afanye uamuzi huo.

"Ninapenda kusema kuwa wazi mimi siondoki Simba, labda wenye Simba yao watake," Mo alisema hayo kwa kifupi.

Mfanyabiashara huyo alisema awali kabla ya kurejea Simba, bajeti yake ilikuwa ni Sh. milioni 600, lakini kwa sasa bajeti hiyo imefikia Sh. bilioni saba anazilipa yeye kutoka katika kampuni zake mbalimbali.

"Bajeti ya Simba imepanda karibu mara 10, mambo yanakwenda sawa sawa, tumesajili wachezaji wa kiwango cha juu, tumeshaanza kufika walipo T.P Mazembe na tutaelekea walipo Al Ahly ambao wanasajili mchezaji hadi kwa bilioni moja," Mo aliongeza.

Aliwataka mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi na wadau wengine wa mpira wa miguu kuendeleza mshikamano kwa sababu Simba itakapofanya vizuri, itazibeba klabu nyingine katika kushiriki mashindano ya kimataifa yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kwa Tanzania kutoa zaidi ya timu moja.

Naye Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema kuwa klabu hiyo iliwahi kupita kwenye wakati mgumu kwa kukosa fedha za kujiendesha, hali ambayo sasa imemalizika.

Manara alisema kwa sasa Simba inaendeshwa kisasa na imekuwa mfano wa kuigwa kwa klabu mbalimbali za ndani na nje ya Tanzania.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
29m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’