Upana wa kikosi wampa jeuri Sven

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Sep 2020
Upana wa kikosi wampa jeuri Sven

Mkufunzi wa klabu ya Simba Sven Vandenbroeck, amesema upana wa kikosi chake utamsaidia kupanga wachezaji kwa kuzingatia mazingira ya uwanja watakaokwenda kucheza mikoani.

Sven alitoa kauli hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu FC katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliofanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, Mbeya, wiki iliyopita.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, Sven alisema viwanja vingi vinavyotumika kwenye michezo ya ligi havina ubora unaomfanya mchezaji kuonesha uwezo wake, ila anashukuru kuwa na kikosi kipana.

"Nina hazina ya upana wa kikosi kitakachonisaidia kupanga wachezaji kulingana na mazingira ya uwanja tunaokwenda kuutumia kwenye kila mchezo wa ligi," alisema Sven.

Alisema anajua mchezo unaokuja na Mtibwa Sugar uwanja watakaotumia wa Jamhuri Morogoro hauna tofauti na waliotoka kucheza dhidi ya Ihefu FC.

"Mashabiki wategemee kuona mabadiliko makubwa ya wachezaji karibia kila mechi kwa kuwa lengo letu ni kutafuta ushindi kwenye kila mchezo ili kuhakikisha tunatetea ubingwa kwa mara ya nne mfufulizo," alisema.

Sven alisema ili wafanikiwe kutetea ubingwa wa ligi, kila mchezo wanatakiwa kuibuka na ushindi, matokeo yatakayoanza kuwajenga waweze kushindana mchezo unaofuata.

Kikosi cha mabingwa hao baada ya kuwasili Dar es Salaam kutoka Mbeya, jana kilianza mazoezi ya kukabiliana na Mtibwa Sugar unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi ijayo.

Baada ya michezo ya mzunguko wa kwanza, Simba inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi tatu sawa na KMC inayoongoza kwa wingi wa mabao ya kufunga.

Azam inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi tatu sawa na Biashara United, Dodoma Jiji, JKT Tanzania na Namungo FC.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
21h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’