Mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere amesema malengo yake ya msimu huu ni kuendeleza rekodi yake ya ufungaji kama alivyofanya misimu miwili iliyopita
Kagere aliondoka na kiatu cha dhahabu katika misimu yote miwili iliyopita baada ya kuibuka mfungaji bora
Msimu wa 2018/19 alifunga mabao 23 na msimu wa 2019/20 akafunga mabao 20
Msimu huu nusura afungue akaunti yake ya mabao kwenye mchezo dhidi ya Ihefu Fc kama sio bao lake kukataliwa na mwamuzi msaidizi
Pamoja na changamoto ya kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza. Kagere amesema atahakikisha anafanya vizuri kila atakapopewa nafasi na kocha Sven Vandenbroeck
"Hesabu zangu ni kuifikia rekodi yangu ya msimu uliopita kwa sababu ndio itasaidia katika timu kupata mafanikio ya kutetea ubingwa"
"Kikubwa kwangu kwa sasa ni kujitoa kwa ajili ya kutimiza majukumu yangu ndani ya timu kwa kuhakikisha timu inapata matokeo chanya kila ninapokuwa uwanjani," alisema Kagere