Kikosi cha timu ya Simba kitaingia kambini kesho kujiandaa na mchezo wa pili ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mtibwa Sugar utakaopigwa siku ya Jumamosi katika Uwanja wa Jamhuri.
Baada ya kurejea jana kutoka jijini Mbeya wachezaji walipewa mapumziko na leo wataanza mazoezi kabla ya kesho kuingia rasmi kambini.
Msemaji wa Mabingwa hao wa nchi, Haji Manara amesema wachezaji wote wapo kamili hata Gerson Fraga ambaye alipewa ruhusa amerejea kikosi na leo atakuwepo mazoezini.
"Wachezaji walipewa mapumziko ya siku moja leo tunaanza mazoezi kesho tunaingia kambini na Alhamisi tunaelekea Morogoro," amesema Manara
ADVERTISE HERE