Simba yaendeleza rekodi ya misimu 13

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Sep 2020
Simba yaendeleza rekodi ya misimu 13

Ushindi wa mabao 2-1 ilioupata Simba Jumapili iliyopita dhidi ya Ihefu FC kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, umeifanya timu hiyo kucheza misimu 13 ya Ligi Kuu bila kupoteza mechi yoyote ile ya ufunguzi

Yalikuwa ni mabao ya John Bocco na Mzamiru Yassin, yaliyotosha kuendeleza rekodi yao safi linapokuja suala la mechi za mwanzo wa ligi.

Mara ya mwisho Simba kupoteza mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu ilikuwa ni 2007/08, ilipochapwa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga.
Ilikuwa ni Septemba 23, kwa bao pekee lililofungwa na Sunday Peter.

Baada ya hapo Simba imecheza kwa misimu yote 13, ikishinda mechi 11 za mwanzo wa msimu na kutoa sare mbili tu.

Rekodi zinaonyesha kuwa mechi zote hizo 13 ambazo Simba imecheza, sita ilicheza ugenini na saba ilianzia nyumbani, huku sare ambazo ilizopata moja ilikuwa nyumbani na nyingine ugenini.

Msimu wa 2008/09, iliichakaza Villa Squad mabao 4-1, kabla ya kuichapa Majimaji mabao 2-0 2009/10, na ikashinda mabao 2-0 dhidi ya African Lyon msimu wa 2010/11.

Simba iliendeleza rekodi yake safi msimu wa 2011/12 ilipoifunga JKT Oljoro mabao 2-0, na African Lyon mabao 3-0 msimu wa 2012/13, kabla ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 ugenini dhidi ya Rhino ya Tabora mechi ya ufunguzi msimu wa 2013/14.

Sare nyingine ya mabao 2-2 ilipatikana msimu wa 2014/15, ilipocheza dhidi ya Coastal Union, huku 2015/16 ikishinda bao 1-0 dhidi ya African Lyon, kabla ya kushinda mabao 3-1 msimu wa 2016/17 ilipoanza na Ndanda FC.

Iliipa kipigo cha mabao 7-0 Ruvu Shooting msimu wa 2017/18, ikaifunga Prisons bao 1-0 msimu wa 2018/19, ikaiadhibu JKT Tanzania mabao 3-1, 2019/20, na Jumapili iliyopita msimu wa 2020/21 ilianza pia kwa ushindi wa mabao 2-1

Kwa hisani ya Nipashe

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’