Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalezi ameweka hadharani vitaumbele vyake vitatu ambayo ataanza navyo katika majukumu yake mapya na mabingwa hao wa nchi
Barbara ambaye uteuzi wake ulithibitishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba juzi, amesema ukubwa wa 'brand' ya Simba unapaswa kwenda sambamba na mapato yanayoingizwa na klabu hiyo
Hivyo moja ya sehemu ambazo ataweka mkazo, ni katika kutafuta vyanzo vipya vya mapato
"Kuna idara za kazi nahitaji kuboresha. Ya kwanza kwenye mapato. Mimi naona Simba ni 'brand' kubwa, lakini kutafsiri kwenye soko ni tofauti. Hivyo kazi yangu ya kwanza ni kutafuta vyanzo vya mapato," amesema
"Lakini pia, nitaongeza wigo wa ushirikiano na vyombo vya habari. Nadhani tunahitaji ushirikiano mkubwa na vyombo vya habari sio tu hapa Tanzania bali Afrika Mashariki, Afrika na duniani kiujumla na tatu ni kupunguza, kubana na kutengeneza ufanisi katika matumizi"
"Jambo la mwisho ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, tunahitaji kuongeza ufanisi kwenye matumizi yetu ya fedha," aliongeza 'Boss Lady' huyo
Barbara alianza majukumu yake ya Utendaji wa Simba tangu mwezi uliopita baada ya Senzo kuondoka. Kabla ya kuthibitishwa, alikuwa akikaimu nafasi hiyo