Simba mwendo mdundo, yaitungua Ruvu Shooting 3-0

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Feb 2018
Simba mwendo mdundo, yaitungua Ruvu Shooting 3-0
Kikosi cha Simba kimeendeleza rekodi ya kupachika mabao mengi katika ligi kuu ya Vodacom baada ya kuichapa Ruvu Shooting mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Uhuru.

Simba iliuanza mchezo huo kwa kasi na iliwachukua dakika 22 tu kupata bao la kuongoza kupitia kwa nahodha John Bocco aliyeunganisha kwa kichwa kona ya Shiza Kichuya.

Mfumo wa 'kubaki' basi haukuweza kuisaidia Ruvu Shooting ambayo wachezaji wake pia walikamia mchezo na kujikuta wakipewa kadi za kizembe.

Kwenye dakika za mwishoni mwa kipindi cha kwanza Simba ilipata pigo baada ya mshambuliaji wake tegemeo Emanuel Okwi kulazimika kutolewa nje baada ya kupigwa kiwiko na Mau Bofu ambaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu.



Kwenye kipindi cha pili Simba ilipunguza kasi ya mashambulizi hata hivyo iliendelea kupeleka mashambulizi ya kushitukiza langoni mwa Ruvu.

Kwenye dakika ya 66, pasi murua ya Shiza Kichuya ilitua mguuni mwa Mzamiru Yassini na kuifungia Simba bao la pili kabla John Bocco hajaifungia tena Simba bao la tatu kwenye dakika ya 76.

Mabao yake mawili aliyofunga leo, Bocco amefikisha mabao tisa sasa akiwa nyuma ya kinara Emanuel Okwi kwa tofauti ya mabao matatu.

Ruvu Shooting walimaliza nane dimbani baada ya Adam Ibrahim kutolewa nje kwenye dakika za majeruhi kwa kuonyeshwa kadi ya pili ya njano.

Matokeo hayo yanaikita Simba kileleni ikiwa na alama 38 huku ikifuatiwa na Azam FC yenye alama 33.

Yanga iko nafasi ya tatu ikiwa na alama 31.

Baada ya mchezo huo Simba itashuka kwenye dimba la Taifa Jumatano Februari 7 kuivaa Azam FC kwenye mchezo mwingine muhimu.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’