Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo Jumapili, Septemba 06 wanaianza kampeni ya kuwania ubingwa wa nne mfululizo kwa kuikabili Ihefu Fc, vijana waliopanda daraja msimu uliopita
Mchezo utapigwa kuanzia saa kumi Alasiri kwenye uwanja wa Sokoine
Simba wako mkoani Mbeya tangu Jumanne ya wiki hii wakijiwinda na mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini
Jana miamba hao wa soka nchini walikamilisha maandalizi yao huku kocha Mkuu Sven vandenbroeck akitamba kikosi chake kuwa tayari kupambana
Huu unaweza kuwa msimu mwingine wa mafanikio kwa klabu ya Simba kutokana na uimara wa kikosi chake
Simba tayari imeweka kibindoni Ngao ya Jamii kwa msimu wa nne mfululizo na leo inaianza kampeni ya kuwania taji la nne mfululizo, ligi kuu ya Vodacom